September 7, 2020

 


KLABU ya KMC leo Septemba 7 imeweza kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru.


Mchezo wa leo umekusanya mabao mengi kuliko mechi zote zilizochezwa jana Septemba 6 ambapo pazia la ligi lilifunguliwa rasmi na mechi saba zilichezwa leo zitachezwa  tatu kukamilisha mzunguko wa kwanza.


Mabao ya KMC yalipachikwa dakika ya 21 kupitia kwa Israel dakika ya 21 akimalizia pasi ya Emmanuel Mvuyekule.


Bao la pili lilipachikwa dakika ya 39 na Hassan Kabunda kwa pasi ya Israel na kuwafanya KMC kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0.


Kipindi cha pili KMC waliendeleza moto wao ambapo dakika ya 57, Abdul Hilary alipachika bao la tatu kwa pasi ya David Bryson na msumari wa mwisho ulipachikwa na Paul Peter dakika ya 74 kwa pasi ya Kabunda.


Kabunda na Israel wametaka leo Uwanja wa Uhuru ambapo wote wamefunga bao mojamoja sawa  na idadi ya pasi ambazo wametoa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic