September 24, 2020

 


KLABU ya Simba imezifunika timu nyingi Afrika ikiwa ni pamoja na Klabu ya Al Ahly ya Misri kutokana  na kushika namba moja kwenye Mtandao wa Istagram.


Hiyo ni kwa mujibu wa Mtandao wa Deporfinanzas ambao umetoa takwimu za mwezi Agosti na kuiweka Simba namba moja kwa umaarufu kutokana na kutembelewa sana na watu.


Takwimu zinaonyesha kwamba kwa mwezi huo watu milioni 536 waliitembelea akaunti ya Simba huku ile ya Al Ahly ilitembelewa na watu milioni 517 na Raja Casablanca watu milioni 511.


Mtandao huo uliandika hivi:"Simba SC ndiyo Klabu maarufu Afrika ndani ya Istagram kwa mwezi Agosti. 


"Hii ni mara ya Kwanza kwa timu kutoka Tanzania kufanya hivi,".

7 COMMENTS:

  1. ✍️ record noted, sasa tutoke Instagram tuingie uwanjani kwenye makombe. Wanasimba wote tuungane tuanze kutwaa makombe ndani ya ligi na kimataifa tujiandae kikosi vzr hakuna lisilowezekana msimbazi. Uwezo tunao, nguvu tunayo na pesa tunazo. Tuachane na wanaojenga kikosi na kubwabwaja hivyo mitaani na mitandaoni eti tunabebwa, bac Afrika nzima wanatubeba mpaka wenyewe utopolo a.k.a Jambo la wageni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Muhimu Kwa sasa wanasimba tuendeleze ule moto wa kupenda kwenda kuingia stadium na kuwapa support wachezaji wetu ili morali isishuke.Bravo wanasimba

      Delete
  2. Jamvi la wageni punguzeni Domo Simba is the another level " barba,mo na wanasimba wote big up👊👊

    ReplyDelete
  3. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo Yanga watasema ni feki au ya Kununuliwa, ni wazi wazi timu hiyo kabisa haijulikani kimataifa na ndio mana hata na ndio mana hata ile kadhia ya Morrison wa Simba hamna kitu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic