DAVID Kissu
kipa namba moja wa Azam FC, ameweka rekodi ya kuwa kipa pekee kwenye Ligi Kuu
Bara kucheza dakika nyingi bila kuruhusu bao lolote ambapo amecheza jumla ya
dakika 360 sawa na mechi nne.
Kissu
alijiunga na Azam FC, akitokea Gor Mahia ya Kenya alipokipiga kwa mafanikio
makubwa akifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Kenya mara mbili kwa sasa
amekuwa nguzo muhimu kwenye kikosi cha Azam ambacho hakijapoteza mchezo wowote
hadi sasa kwenye Ligi Kuu Bara.
Kisu
amekusanya ‘clean sheet’ hizo kwenye mechi dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal
Union, Mbeya City na Tanzania Prisons ambapo amecheza kwa dakika 90 kwenye
mechi zote.
Azam FC
inashika nafasi ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara wakikusanya jumla ya pointi 12,
kwenye mechi nne walizoshuka dimbani huku wakifunga jumla ya mabao matano na
wakiwa hawajaruhusu bao lolote hadi sasa.
Akidumu hivyo mpaka mechi kumi na saba atakua kipa bora ila ifahamike tu kwamba kipa bora huanza na mabeki bora,bado mapema ligi haijachanganya mtakuka kumtafuta kwa tochi huyu.
ReplyDeleteSasa kaweka Record hapo jamani, mbona unapenda sana kudanganya umma? Acha unaa
ReplyDelete