UONGOZI wa KMC umesema kuwa kupoteza kwao mchezo wao wa kwanza mbele ya Kagera Sugar kwa kufungwa bao 1-0 hakujawatoa kwenye ramani kwani ni sehemu ya mchezo wanajipanga kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Polisi Tanzania.
KMC ilifanikiwa kucheza mechi tatu ambazo ni dakika 270 bila kupoteza ambapo iliweza kuongoza raundi ya kwanza mpaka ya tatu kabla ya raundi ya nne kupokewa na Azam FC ambao wana pointi 12 kibindoni huku wao wakibakiwa na pointi tisa wakiwa nafasi ya tatu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wanaweka kando matokeo yao yaliyopita na kuanza kuivutia kasi Polisi Tanzania watakayokutana nayo Oktoba 5, Uwanja wa Uhuru.
“Tulipoteza mchezo wetu uliopita mbele ya Kagera Sugar, imetuumiza kwa kuwa tulianza bila kupoteza hivyo tunaanza tena kurejea kwenye ule moto wetu ambao tulianza nao kwani kikosi chetu kipo imara na tutapambana kufikia malengo yetu.
“Mashabiki tunakila sababu za kuwashukuru kwa kuwa wamekuwa nasi bega kwa bega ila hatujakata tamaa tunaamini kwamba mchezo wetu ujao lazima tutarejesha ile kasi yetu.
"Tunarudi nyumbani na tutakutana na Polisi Tanzania, hapo tutafanya vema ili kupata pointi tatu muhimu nina amini kwamba mashabiki wataendelea kuwa nasi hivyo wasikate tamaa waendelee kuwa pamoja nasi," amesema Christina.
Polisi Tanzania imeshinda mchezo wake uliopita kwa mabao 3-0 mbele ya Dodoma Jiji, mchezo uliochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.
0 COMMENTS:
Post a Comment