RONALD Koeman, Kocha Mkuu wa Klabu ya Barcelona jana Agosti 31 alianza kukinoa kikosi chake kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2020/21 bila ya uwepo wa nyota wao Lionel Messi.
Baada ya kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Quique Setien, Koeman alikabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi hicho ambacho kilitoka kupokea kichapo cha udhalilishaji cha mabao 8-2 mbele ya Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Picha ambazo zilipigwa na kuwachukua wachezaji ambao walikuwa wameanza mazoezi zilimuonyesha kocha huyo akiwa na baadhi ya wachezaji ambao wanajiandaa na kuanza kwa La Liga huku Messi akiwa hayupo.
Wachezaji wa Barcelona walipigwa picha wakiwa mazoezini ambapo winga Ousmane Demebele alionekana akikimbia huku akitumia vifaa vipya vya mazoezi vya timu hiyo.
Pia, Gerard Pique alionekana akiwa na mpira akichezea kwenye mazoezi hayo ambayo yalifanyika bila ya uwepo wa Messi ambaye inaelezwa kuwa anahitaji kuondoka ndani ya timu hiyo na inatajwa kuwa anahitaji kwenda kucheza Manchester City inayoshiriki Ligi Kuu England.
0 COMMENTS:
Post a Comment