September 28, 2020

 


BLACK Leopard ya Afrika Kusini imempa dili la miaka mitatu, Patrick Aussems kukinoa kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21.


Aussems raia wa Ubelgiji alikuwa Kocha Mkuu wa Simba alipigwa chini mazima msimu wa 2019/20 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwa kusimamia nidhamu ndani ya kikosi hicho.

Akiwa Simba aliweza kutwaa taji ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 na alifanikiwa kukiongoza kikosi hicho kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Anatarajiwa kuwasili nchini Afrika Kusini wiki ijayo kwa ajili ya kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kipya.
 
Aussems ameiambia City Press kuwa :"Muda mrefu nilikuwa nahitaji kufanya kazi Afrika Kusini, ninafuraha ya kupata kazi huko ninaamini nitafanya vizuri.

"Ligi ya Afrika Kusini imekuwa kubwa na ni maarufu ukianzia kwenye miundombinu mpaka ukusanyaji wa taarifa na timu imeonekana ikipambana hivyo nitakwenda nayo sawa."

Msimu wa 2019/20, timu hiyo ilimaliza Ligi Kuu ya Afrika Kusini ikiwa nafasi ya 15 na pointi zake 29 baada ya kucheza mechi 30.

3 COMMENTS:

  1. Huyu Kipindi yupo Simba alikuwa anasema kila wiki anapokea ofa kibao, imekuwaje akose timu mpaka leo?

    ReplyDelete
  2. Sven yupo vizuri na kikazi zaidi kuliko Ausems.Bwana mdogo lakini anamsiamo wa taalima ya kazi yake na wachezaji wa simba wakiyakubali malezi yake basi wanaweza kwenda kufanya kazi klabu yeyote nje na ndani ya nchi na wakafanikiwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic