September 23, 2020

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotić amewapa majukumu mapya washambuliaji wake Michael Sarpong na Yacouba Sagne kwa kuhakikisha wanafunga bao katika kila mchezo kwa kuwa anaamini yatakuwa na msaada mkubwa kwao.

 

Mserbia huyo ametoa kauli hiyo kufuatia timu yake kufunga mabao matatu katika mechi tatu licha ya kuwa na pointi saba katika msimamo wa ligi kuu.


Krmpotić amesema kuwa ana kila sababu za kuwataka washambuliaji wake wakiwemo Michael Sarpong na Yacouba Sogne kuhakikisha wanafunga mabao katika kila mchezo ili kuweza kujiweka katika mazingira mazuri kutokana na ushindani uliopo.

 

“Wakati mwingine matokeo ya ushindi ni mazuri kwetu kwa kuwa yanatusaidia kufikia malengo japo kuwa bado hatujafikia kwenye ubora ambao kila mmoja wetu angependa kuona tukicheza hasa kwenye kufunga mabao.


“Tumekuwa na idadi ndogo ya mabao ya kufunga tangu tuanze ligi na ni tatizo ambalo tunalifanyia kazi kwa kuhakikisha washambuliaji wetu wanafunga mabao ya kutosha kutokana na nafasi ambazo zitapatikana kwa sababu kama tunaweza kushinda kwa kupata pointi tatu bila ya mabao mengi huenda ikawa shida kwetu huko mbele hivyo lazima wabadilike,” amesema Krmpotić.

8 COMMENTS:

  1. Muda utaongea, tuwe na subira, muda upite, ukifika wakati utahukumiwa kwa muda ulio kaa hapo. Time will tell.

    ReplyDelete
  2. Sababu ni hizo kwa hizo zikijirejea kama wimbo, tuazipatia dawa lakini mgonjwa yupo palepale. Tokea Zahera, Mbelgiji na huyu tulionaye

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnataka mnunuliwe mechi kama mikia. Acheni timu ipambane wanjani. Wenzenu wanawapumbaza wanachama wao wasidai 20 Bilioni. Msikubali kuwa wajinga kama wao

      Delete
    2. Ndiyo uwezo wako ulipofikia! Je na Kagera Yanga imenunua? Gsm ni nani Yanga na anafanya maamuzi yote? Si lazima kuchangia kila kitu wakati mwingine waachie watu wenye mawazo ya kujenga badala ya kukaririsha watu.

      Delete
  3. Haya maelezo ya Kocha yamejirudia sana, kwa sasa yanatosha.
    Tatizo ninavyo liona lipo kwenye mfumo anaouingiza kutumika na kupwaya kwa kiungo mchezeshaji.
    Nina wasiwasi pia na msaada anaoupata kutoka kwa Kocha Msaidizi.
    Ningemshauri kocha atumie mfumo mwepesi na rahisi kutumika (442), ili aendelee kupata ushindi wakati huo huo akiendelea kujenga mifumo mipya.
    Uchezaji wa timu yake kea sasa sio rafiki kwa washambuliaji! Mwambusi alipaswa kumwambia haya hasa anapocheza na zile timu zinazochezea kupata sare (kujiangusha/kupoteza muda)

    ReplyDelete
  4. Mpira wa miguu sio rede, lazima team ikae kwa muda ilikupata combination ( chemistry), sasa wadiojua mpira ndio wanacomment kiushabiki maandazi.

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. Makocha wa South Africa (Kocha wa Fitness-Riedoh Bierden na Cassien Kocha wa Physio) Swali, Je, wamerudi kambini kuungana timu ili kujenga timu? Swali pia linabaki, kwanini waliondoka wakati huu ambapo ligi inaanza na timu inahitaji utaalamu wao? Utawapaje likizo wafanyakazi wakati uzalishaji unaendelea? Je kiwango cha fitness kikipungua Viongozi wa Yanga pamoja na GSM hawaoni watakuwa wamewakosea mashabiki kwa kutoa ruhusa kwa watu muhimu katika benchi la ufundi kuondoka katika muda ambao wanahitajika? Je, ni lini watarudi na kuungana na timu? Je, hawaoni kuwa kuna hujuma na mkakati wa kisayansi kuidhoofisha Yanga unaofanywa na wanayanga wenyewe?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic