July 3, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka jambo kuhusiana na aliyekuwa mchezaji wake, Mzambia, Obrey Chirwa ambaye hivi sasa amejiunga na Ismailia ya Misri.

Kwa mujibu wa Hussein Nyika kupitia kipindi cha michezo, Radio One, amesema Chirwa alimaliza mkataba na Yanga hivyo wasingeweza kumzuia asifanya mazungumzo na timu zingine.

Nyika amefunguka kwa kusema yeye kama kiongozi wa Yanga na klabu kwa ujumla wanamtakia kila lililo jema huko alipo katika kazi yake ya mpira baada ya kufikia mwafaka na timu yake mpya ya Ismailia kuichezea.

Mbali na kuondoka kwa Chirwa Yanga, Nyika amesema mchezaji huyo alikuwa ni moja ya waliokuwa bora kwenye kikosi cha timu yao kutokana na mchango pamoja na umahiri wake ndani ya Uwanja.

Chirwa ameondoka Yanga akiwa amechangia kuipatia ubingwa wa Ligi Kuu Bara katika msimu wa 2016/17 mbele ya watani zao wa jadi Simba ambao waliambulia nafasi ya pili.

6 COMMENTS:

  1. Kama chirwa alimaliza mkataba sasa yanga ilikuwa na figisu za nini za kuibania Simba wasimsajili mchezaji huru na walokuwa hawana uwezo nae tena wa kumuhudumia wameona bora akasajili nje ya Tanzania bure kabisa bila ya Yanaga kunufuika na chochote kile? Pengine kama Simba ingemsajili Chirwa isingeweka nguvu tena kwa Kagere kitu ambacho labda Yanga ingekuwa na nafasi ya kumdaka. Roho mbaya mara nyingi huwa ubaya unakurudia na kukutafuna kwenye kidonda waacha Yanga wapate taabu kwani wananijijengea wenyewe mazingira ya tabu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba hawakuwa na nguvu ya kipesa ya kumsajili ndio maana Yanga wakambania mpaka mkataba wake ulipoisha. Unadhan km dau lingewekwa mezani Yanga wangeliacha? Tatizo tunashabikia kitu bila kuona uhalisia wake kwa undani wa jambo husika. Simba kelele nyingi kama mmechukua ubingwa Mara 5 mfululizo hivi.

      Delete
    2. Simba hawakuwa na nguvu ya kipesa ya kumsajili ndio maana Yanga wakambania mpaka mkataba wake ulipoisha. Unadhan km dau lingewekwa mezani Yanga wangeliacha? Tatizo tunashabikia kitu bila kuona uhalisia wake kwa undani wa jambo husika. Simba kelele nyingi kama mmechukua ubingwa Mara 5 mfululizo hivi.

      Delete
  2. Kama uwezo wa kipesa haupo mbona wamemsajili Kagere?

    Protas Iringa

    ReplyDelete
  3. KWAHIYO MWANDISHI UCHWARA ULIKUWA UNAJARIBU KUELEZA NN LABDA,AU NDIO UNAJAZA PEJI ILIMRADI UPATE WAFUASI NA KUPATA MATANGAZO KWA WENYE HELA? UNA SAFARI NDEFU YA KUJIKWAMUA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkubwa si usisome tu makala zake? Au uanzishe blog yako itakayokuwa perfect. Una gubu sanaaaa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic