September 24, 2020


ZLATKO Krmpotic, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wanajukumu kubwa moja la kufanya kwenye mechi zao zote zilizobaki kufunga mabao mengi yatakayowapa nafasi ya kuwa na mwendelezo mzuri kwenye mechi zinazokuja.

Kwa sasa Yanga imecheza mechi tatu za ligi imefunga mabao matatu na kufungwa bao moja huku kibindoni ikiwa na pointi saba baada ya kukamilisha raundi ya tatu nafasi yake ni ya tano.

Ilianza kwa sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons kisha ikaambulia ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City na kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar.

Raia huyo wa Serbia amesema:"Kikubwa tunahitaji ushindi kwenye mechi zetu hilo ni jambo la kwanza pia kwa kuwa tumekuwa na tatizo la kufunga mabao mengi jukumu lingine ni kuongeza umakini katika kutengeneza nafasi na kuzimalizia pia.

"Kwa kufanya hivyo tutakuwa imara na kujiongezea hali ya kujiamini kwa wakati ujao muhimu kuwa na ushindi na kufunga mabao mengi."

Kwa sasa Yanga ipo kwenye maandalizi ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mabao ya Yanga yamepachikiwa kimiani na Lamine Moro ilikuwa mbele ya Mbeya City, Michael Sarpong mbele ya Tanzania Prisons na Mukoko Tonombe mbele ya Kagera Sugar.

8 COMMENTS:

  1. UTOPOLO UTD bwana mnadhan ligi ize?

    ReplyDelete
  2. Kosa kumuacha molinga jamaa bonge la fowadi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. True! Molinga huyoo Zesco kimataifa utopolo wamebaki mavumbini anatapatapa tu na Tena tshitshimbi naye Tyler svital utopolo wamebaki kuomba taarabu na kutuonesha blauzi za pampers tu.

      Delete
  3. Tupeni raha sisi mashabiki wenu wachezaji mshasajili vizur. kinachotakiwa twataka ushindi

    ReplyDelete
  4. Zesco ameshika nafasi ya 5 Hana mashindano yeyote ya kimataifa so acha kuudanganya umma kenge
    wewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa we na Zesco Nani Bora, acha umkiazi muda wowote wanauhakika kucheza kimataifa. We mpaka mbeleko za simba.Mwaka huu tutawabeba Tena ninyi mdebwedo.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic