September 7, 2020


 MABONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Hassan ‘Twaha Kidudu na Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe’ wanatarajia kupanda ulingoni tena Desemba 26, mwaka huu kuzichapa katika pambano la usiku wa mabingwa.

Pambano hilo limepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Club Next Door, Masaki jijiji Dar.


Kiduku na Dulla Mbabe ambao wametoka kupigana wikiendi iliopita wapanda ulingoni katika pambano kwa kucheza na mabondia kutoka nchini Malawi.


Mbali ya mabondia hao, mabondia  wengine watakaopanda ulingoni ni Mfaume Mfaume atazichapa na Chikondi Makawa wa Malawi,  wakati  Dullah Mbabe yeye akitarajia kuzichapa na  Arick Mwenda pia kutoka Malawi.


Kwa upande wa Selemani Kidunda kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ akitarajia kucheza dhidi ya  Limbani Masamba na mwenzake  Ismail Isaac ‘Gari ya Tano’  atacheza na  bondia wa ndani Baina Mazora huku Tonny Rashid atetea mkanda wake kwa Mzimbabwe, Tinashe Mwadziwana .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic