September 23, 2020

 






MZUNGUKO wa tatu kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara umekamilika kwa ushindani mkubwa ambapo kila timu imeonesha ushindani mkubwa kusaka pointi tatu muhimu.


Mechi moja pekee ilimaliza dakika 90 bila nyavu kutikiswa ilikuwa ni kati ya Coastal Union v Dodoma FC,  Uwanja wa Mkwakwani.


Jumla yamefungwa mabao 14 na timu iliyofunga mabao mengi mzunguko wa tatu ni Simba ambayo ni mabao manne.


Jumla ya supa sub wawili wamepatikana ndani ya mzunguko wa pili ambapo wa kwanza aliyewapoteza wote ni Relliants Lusajo wa KMC ambaye aliingia kwenye mchezo dhidi ya Mwadui FC dakika ya 50 akichukua nafasi ya Emmanuel Mvuyekule.


Alitupia kimiani mabao yote mawili ndani ya 18 ambapo wakati akiingia timu yake ilikuwa nyuma kwa kufungwa bao 1-0 na Mwadui FC ambayo haijawa na mwanzo mzuri.


Chris Mugalu naye anaingia kwenye orodha ya super sub ndani ya mzunguko wa tatu ambapo alifunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa aliingia dakika ya 76 akichukua nafasi ya Meddie Kagere na alifunga bao dakika ya 84.


KMC kwa sasa ni vinara kwa mzunguko wa tatu kibindoni wana pointi 9 na wamecheza mechi tatu huku wakitupia mabao nane na kufungwa mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic