September 24, 2020

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amependezwa na ufundi wa kiungo wake Clatous Chama huku akibainisha kuwa ni ngumu kwa kiungo huyo kubakia klabuni hapo.

Chama ndiye anashikilia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo aliitwaa msimu uliopita baada ya kuonyesha makali.

 

Amekuwa ndiye mchezaji mahiri zaidi kwenye kikosi cha Simba kuanzia alipojiunga nacho akitokea Power Dynamos ya nchini Zambia.


Sven ambaye amekuwa ni mtu mwenye msimamo mkali, amesema ni ngumu kumbakiza staa huyo Msimbazi kwa sababu ya kiwango anachokionyesha lakini pia mkataba wake unamalizika mwakani wakati ligi itakapomalizika.

 

Chama alijiunga na kikosi cha Simba mwaka 2018, ambapo mkataba wake utaisha Juni mwakani na kumpa uhuru wa kusajiliwa na timu nyingine.

 

Sven amesema: “Ni maamuzi yake mwenyewe kuendelea kubaki Simba kwa mwaka huu wa mwisho wa mkataba na kila mchezaji anaweza kufanya atakachoamua.


“Ningependa aendelee kubaki Simba lakini akiendelea na kiwango hiki itakuwa ngumu kumbakisha kwenye timu hii.


“Tusubiri tuone, sijui nini kinaendelea akilini mwa Chama au bodi, lakini akiendelea hivi mpaka mwisho wa mkataba nitakuwa na furaha sana kwa kuwa ni mchezaji mahiri.

 

“Uamuzi kwenye hali ya kiuchumi ya soka ilivyo sasa hivi, haupo kwa Chama mwenyewe kwa kuwa mchezo huu sasa ni biashara, hivyo tusubiri tuone nini kitatokea,” alisema kocha huyo baada ya mechi dhidi ya Biashara United ambayo kiungo huyo alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao.

 

Simba iliwapiga Biashara United kichapo cha mabao 4-0 na kufikisha pointi saba baada ya mechi tatu walizocheza msimu huu.


7 COMMENTS:

  1. We ni yanga tunakufahamu,kocha alisema ataongea na viongoz wa mwongeze mkataba chama haraka iwezekanavyo lkn wewe unasema itakuwa ngumu chama kubaki au wewe ni wakala wake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Natamani kukuelimisha muda tu ndio sina

      Delete
    2. Kitu gani utakacho mueleimisha zaidi ya wivu tu na kutamani chama aondoke simba ili iwe afadhali kwenu dua la kuku halimpati mwewe

      Delete
  2. Nyota yke imeng'aa zaid akiwa simba haina ubixhi cha msing atulie aongezewe kandaras aendelee kuitumikia klabu kwa mafanikio zaid

    ReplyDelete
  3. Simba wajitahidi wampe mkataba ili hata ikibidi kuhama basi wafanye biashara, sio kumeacha aondoke akiwa huru

    ReplyDelete
  4. Ila mkataba haujaisha na yeye hajasema haongezi mkataba

    ReplyDelete
  5. Mda ukifika ataondoka tu maana mpira ni kazi yake na hakuna mchezaji wa kukaa timu moja milele, kwahiyo MISUKULE fc tulieni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic