September 22, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo utashusha kikosi kizima cha kazi kwa ajili ya kushinda na kutoa burudani mbele ya African Lyon kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, majira ya saa 10:00 jioni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wamejipanga kuendelea kutoa burudani na kushinda mchezo wao mbele ya African Lyon.

"Kawaida ya Simba ni moja siku zote kucheza mpira mzuri ambao utatoa burudani na matokeo chanya kwenye mchezo wetu ambao tunacheza bila kujali ni aina gani ya mchezo.

"Hii ni njia bora kwetu itakayotufanya tuwe bora na kwenye mchezo wetu dhidi ya African Lyon ni mahususi kwa ajili ya wale wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kucheza muda mrefu pamoja na kuendelea kuifanya timu kuwa bora.

"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa kuwa kiingilio ni cha kawaida sana na tunazidi kuwashukuru kwa kuwa wamekuwa wakitupa sapoti mara kwa mara hivyo wasichoke katika hili," amesema.

Miongoni mwa nyota wa Simba ambao hawajapata muda mwingi wa kucheza ndani ya Simba ni pamoja na Chris Mugalu, Rarry Bwalya, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu na Beno Kakolanya.

8 COMMENTS:

  1. Wiki iliyopita Yanga walipoandaa mechi ya kujaribu mifumo waliambiwa wanatafuta nauli ya kwenda Bukoba sasa sijui hii ya Simba nayo ni ya kutafuta nauli au vipi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga waliweka kiingilio sh. elfu tano kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege pale Chamazi, na wakaitangaza kweli kweli. Hii inaonyesha kuwa walikuwa wanatafuta hela. Lakini mechi hii ya Simba dhidi ya Lyon haijatangazwa sana wala hakuna anayepiga kelele kuwaita mashabiki waende Chamazi, na hata kiingilio hakijulikani

      Delete
    2. Utakuwa upo Sudan Kusini wewe,mechi imetangazwa na vyombo vyote vya habari halafu unasema haijatangazwa?hawajaweka wazi kiingilio maana wanasikilizia hali itakuaje kwa hiyo wanapima upepo kwanza

      Delete
    3. Viingilio viliwekwa tangu jana na viko wazi kabisa - VIP 5,000/- na mzunguko ni 3,000/-

      Delete
  2. Kutoa burudani na sio kuombs fedha jaman

    ReplyDelete
  3. Lengo la mechi hii ya kirafiki dhidi ya African Lyon ni kutoa burudani na pia kuwaweka fit wachezaji na hasa wale ambao hawajapata nafasi ya kucheza. Suala la fedha kwa Mnyama sio issue

    ReplyDelete
  4. Utopolo na wengine mkumbuke Simba anajiandaa kimataifa, tunamtaka tuwabebe tena mkashiriki kimataifa hivihivi hamwezi. Acheni midomo endeleeeni kushangaa mwendokssi jangwani tukiwatengenezea njia mtoke huko kwa huruma yetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic