ABDULKARIM Amin, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa wanahitaji kushinda kwenye mechi zote msimu huu ikiwa ni pamoja na mchezo wao wa leo Oktoba 4 dhidi ya Kagera Sugar.
Tayari Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba imeshinda mechi nne ndani ya dakika 360, leo inashuka Uwanja wa Azam Complex kuwakabili Kagera Sugar majira ya saa 1:00 Uwanja wa Azam Complex.
Azam FC imejikusanyia mabao matano kwenye mechi nne na pointi zake ni 12 kibindoni ikiwa nafasi ya pili inakutana na Kagera Sugar yenye pointi nne na imefunga bao moja ikiwa nafasi ya 12.
Amin amesema :”Baada ya kushinda mechi zetu mbili ugenini mbele ya Mbeya City na Tanzania Prisons tunarejea nyumbani,malengo makubwa ni kushinda kwenye mechi zetu tutakazocheza ili kupata pointi tatu muhimu,”.
Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa wanahitaji pointi tatu na watapambana kupata matokeo.
0 COMMENTS:
Post a Comment