UONGOZI wa timu ya Coastal Union umesema kuwa utaifunga Yanga katika mchezo utakaochezwa leo, Oktoba 3 Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa maandalizi ya kikosi yapo vizuri na wanaamini watapata pointi tatu kwenye mchezo huo.
“Kikosi kipo vizuri mpaka muda huu hakuna majeruhi tunamshukuru Mungu. Vijana wana morali kubwa na shauku ya kuendelea kupata ushindi hivyo imani yetu ni kwamba ili tupate huo ushindi ni lazima tufunge na hicho ndicho tutakachokifanya.
“Tumejiandaa vizuri na lengo letu ni kuendeleza ushindi wetu tulioupata dhidi ya JKT Tanzania kwa ushindi wa bao 1-0, tunajua Yanga ni timu kubwa na ina mashabiki wengi.
"Mashabiki wetu pia tunawaomba wajitokeze kuona namna gani tutafanya uwanjani kwa uwezo tunao na nguvu pia, tumetoka kushinda tunajiamini na tunaamini kwamba inawezekana kushinda tunahitaji pointi tatu," amesema.
Coastal Union imepoteza mechi mbili ndani ya ligi na kupata sare moja na kushinda mchezo mmoja ambapo mechi ya kwanza walifungwa na Namungo FC bao 1-0 na mechi ya pili walifungwa na Azam wana lambalamba mikwaju 2-0 na walitoka sare dhidi ya Dodoma jiji ambapo walitoshana nguvu ya bila kufungana huku wakishinda mbele ya JKT Tanzania kwa ushindi wa bao 1-0.
Wanakutana na Yanga ilyoshinda mechi tatu na kupata sare moja mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungana bao 1-1 Uwanja wa Mkapa.
MUNGU AWPE NGUVU
ReplyDelete