HASSAN Kessy, beki matata ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar ambaye aliwahi kucheza pia ndani ya Yanga kwa sasa anapata tabu ndani ya Mtibwa Sugar kwa kuwa timu yake imekuwa na mwendo wa kusuasua ndani ya Ligi Kuu Bara.
Akiwa ameanza kikosi cha kwanza mechi tatu mbele ya Ihefu FC Uwanja wa Sokoine wakati timu yake ikishinda bao 1-0 kisha alishuhudia timu yake ikiyeyusha pointi tatu mbele ya Yanga Uwanja wa Jamhuri kwa kufungwa bao 1-0.
Akiwa hajapoa Kessy alianza kikosi cha kwanza mbele ya Biashara United, Uwanja wa Kirumba na kushuhudia timu yake ikitunguliwa bao 1-0.
Akiwa ametumia dakika 270 ameyeyusha dakika 180 ambazo ni mechi mbili kushuhudia timu yake ikichapwa na dakika 90 alitumia kushangilia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 ikiwa imecheza mechi 5 imeshinda mechi moja, ikiwa na sare mbili sawa na zile ilizopoteza ambazo ni mbili.
Ofisa Habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru amesema kuwa wanaamini watarejea kwenye ubora wao kwenye mechi zao zijazo mashabiki wasikate tamaa.
Kesho Oktoba 15 ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Gwambina FC mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kwa kuwa Gwambina imetoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya Ihefu huku Mtibwa Sugar ikitoka kupoteza mbele ya Biashara United.
0 COMMENTS:
Post a Comment