October 14, 2020


 YANGA ikiwa imetupia jumla ya mabao saba kwenye mechi zake tano za Ligi Kuu Bara, mzawa Deus Kaseke ametoa pasi moja ya bao ilikuwa wakati Yanga ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union,  Oktoba 3.


Pasi nyingine zote zimetengenezwa na wageni pamoja na mabao ndani ya Yanga ilikuwa namna hii:-


Bao la Haruna Niyonzima raia wa Rwanda ngoma ilikutana na mikono ya kipa wa Coastal Union asisti ikafa.

Bao la Yacouba Songne raia wa Burkina Faso asisti ilikuwa ya Tonombe Mukoko raia wa Congo. 


Bao la Carlos Carlinhos raia wa Angola asisti ilikuwa ni ya Kaseke, hii ilikuwa ni Oktoba 3, Uwanja wa Mkapa.


Wakati Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, bao la Lamine Moro wa Ghana,  asisti ya Carinhos.


Wakati Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar,  bao lilifungwa na Tunombe Mukoko asisti ya Tuisila Kisinda wote wa Congo. 


Wakati Yanga ikishinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City bao la Lamine asiti ya Carinhos. 


Yanga inalazimisha sare ya kufungana na Tanzania Prisons  1-1 Sarpong alipachika bao baada ya mabeki kujichanganya na pasi iliyopigwa na Farid Mussa.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic