October 14, 2020


 KOCHA Mkuu wa Azam FC, Mromania, Aristica Cioaba amesema kuwa hawezi kuwa na presha yoyote kutoka kwa wapinzani wake wakiwemo Simba na Yanga kwa kuwa wao ndiyo wanaongoza ligi.

 

Azam inaongoza ligi ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi tano, ambazo imeshinda zote ikifuatiwa na Simba wenye pointi 13, sawa na Yanga ambao wanatofautiana kwa mabao ya kufunga katika mechi tano walizocheza msimu huu.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Cioaba alisema kuwa kwa upande wao wamejipanga kuendelea kupata matokeo katika kila mchezo utakaokuwa mbele yao bila ya kuangalia kasi ya wapinzani wao.

 

“Hatuwezi kuwa na presha kwa sababu tumejipanga na tumelenga kushinda kila mchezo ambao upo mbele yetu na hilo ndiyo jambo kubwa kutokana na ugumu na ushindani wa ligi ulivyo, hatuhitaji kuonyesha kushindwa.

 

“Naamini timu yangu ina wachezaji wazuri na bora ndiyo maana hatuhitaji kuwa watu wa presha kwa sababu tunataka kufi kia malengo ya msimu huu ndani ya timu, hakuna haja ya sisi kucheza kwa presha yoyote zaidi tunaangalia kupata matokeo kwenye mechi zetu,” alisema Cioaba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic