October 7, 2020

 


KUFUATIA Kikosi cha Ihefu kuendelea kupata matokeo mabovu, muda mfupi kabla ya kufutwa kazi, jana Oktoba 6 aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Maka Mwalwisi ameibuka na kudai kuwa timu yake haikupata muda mzuri wa kujiandaa vya kutosha kuelekea kuanza kwa msimu huu wa 2021/21.

 

Mwalwisi alitoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika mchezo wa mzunguko wa tano ambao ulikuwa ni wa mwisho kwake kukaa kwenye benchi la ufundi ilikuwa ni kwenye mchezo dhidi ya Gwambina FC na kukubali kipigo cha mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

 

Mwalwisi amesema:-"Wote ni mashahidi kuwa sisi tulipanda kupitia 'play-off' na tulivyopanda tulijikuta tuna muda mchache sana wa kuandaa kikosi kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara ambayo nayo ilikuwa imechelewa kuanza kutokana na Janga la Virusi vya Corona ambalo lilikumba ulimwengu wote," alifafanua.

 

Aliongeza kwa kusema kuwa hakukuwa na muunganiko mzuri kwenye kikosi chake jambo ambalo lilimfanya ashinwe kupata matokeo chanya.


Mchezo wake wa kwanza alikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Simba, Uwanja wa Sokoine, alishinda bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting na alifungwa mabao 2-0 mbele ya Mtibwa Sugar.


Kwa sasa Ihefu ipo kwenye mchakato wa kumsaka kocha mpya atakayebeba mikoba ya kocha huyo. 


Ni miongoni mwa timu zenye usafiri mzuri na ofisi bomba pale Mbeya.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic