October 16, 2020


 IKIWA Simba ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi tano na kujikusanyia pointi 13 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu, kocha mkuu wa kikosi hicho, Sven Vandenbroeck, amesema sababu kubwa inayompa nafasi Aishi Manula kukaa golini ni uwezo wake.

 

Manula amekaa golini kwenye mechi zote tano ambazo Simba imecheza mpaka sasa kwenye ligi, huku kipa namba mbili wa kikosi hicho, Beno Kakolanya akiendelea kusugua benchi bila ya kupata nafasi hata ya kudaka kwa dakika moja.


Kwenye mechi hizo tano, Manula ameruhusu mabao mawili na kuondoka na clean sheet tatu mbele ya Biashara United, Gwambina na JKT Tanzania.

 

Aliruhusu mabao dhidi ya Ihefu na Mtibwa. Sven amesema: “Kufanya vizuri kwa Manula ni sababu ya yeye kuendelea kukaa langoni, lakini haina maana kwamba wengine hawawezi kufanya vizuri, ni suala la kusubiri wakati kuona kwao itakuwaje.”


Kakolanya baada ya kutua Simba akitokea Yanga ambapo alikuwa ni kipa namba moja msimu wa 2018/19 hajawa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza.


Msimu wa 2019/20 alipotua Sven alianza kumpa nafasi kikosi cha kwanza ila baadaye alimrejesha tena benchi na kuanza kumpa nafasi Manula ilikuwa baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Uhuru.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic