October 16, 2020


 HUENDA mashabiki wa soka nchini Uingereza wanaweza kurejea tena viwanjani hivi karibuni, baada ya ombi la mashabiki kupata saini nyingi kutoka kwenye Bunge la Uingereza ambalo limepanga kuijadili taarifa hiyo Novemba 9, mwaka huu.

 

Tangu Machi, Serikali ilipiga marufuku mashabiki kuingia viwanjani kutokana na ugonjwa wa Corona, hivyo hatua hiyo endapo itafikiwa ni nafuu kwa vilabu vingi ambavyo vinategemea zaidi mapato ya mlangoni kuendesha klabu zao.

 

Licha ya kuchezwa bila ya mashabiki, ligi hiyo imeendelea licha ya ukweli kuwa  imepungua msisimko na ladha, ambapo mpaka sasa zimechezwa raundi nne.  


Timu ya  Everton inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 12 wakishinda mechi zote  nne walizoshuka dimbani.


2 COMMENTS:

  1. Hii sijui kama itawezekana maana sehemu nyingi za ulaya covid-19 imeibuka upya na baadhi ya miji ya uengereza tayari iko kwenye lock down. Mji wa Liverpool nafikiri tayari uko kwenye lock down.

    ReplyDelete
  2. Hii sijui kama itawezekana maana sehemu nyingi za ulaya covid-19 imeibuka upya na baadhi ya miji ya uengereza tayari iko kwenye lock down. Mji wa Liverpool nafikiri tayari uko kwenye lock down.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic