October 7, 2020


 

KOCHA Mkuu wa Mbeya City, Amri Said amesema kuwa bado anakijenga kikosi kutokana na kukosa wachezaji wenye uzoefu pamoja na ushindani kuwa mkubwa kwenye Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

 

Sare ya bila kufungana aliyoipata mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Sokoine raundi ya tano inawafanya wavune pointi moja ndani ya ligi.

Hiyo inakuwa pointi ya kwanza msimu huu kwa Mbeya City ambayo imekuwa na msimu mbovu na inaburuza mkia baada ya kucheza mechi tano ina pointi moja kibindoni na safu yao ya ushambuliaji haijafunga bao mpaka sasa.

 

 Kocha Mkuu wa Mbeya City, Amri Said amesema:- “Wachezaji wangu wanapambana kwenye mechi zote lakini kuna ugumu katika kumalizaia nafasi ambazo wanazitengeneza kwenye mechi zetu.


"Kuna ushindani mkubwa ndani ya ligi hilo lipo wazi na kila mmoja anatambua kwa mwenendo ambao tupo nao tunazidi kuimarisha kikosi ili kupata matokeo chanya, kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti."

 

Mbeya City ilianza kunyooshwa kwa mabao 4-0 mbele ya KMC Uwanja wa Uhuru na ilifungwa bao 1-0 mbele ya Yanga, Uwanja wa Mkapa na iliporejea Mbeya ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Namungo na ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Azam FC.


Pointi moja imepata kwenye sare ya bila kufungana mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine.


Kwenye mechi tano ambazo imecheza imeruhusu kufungwa mabao 7 ndani ya dakika 450.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic