MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil, Neymar, amesogea hadi nafasi ya pili ya wafungaji bora wa muda wote kwa kufikisha magoli 64 akiwa nyuma ya mkongwe Pele mwenye magoli 77.
Idadi hiyo ameifikisha baada ya kufunga hat trick dhidi Peru ambapo walishinda kwa magoli 2-4 katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.
Nyota huyo wa PSG mwenye miaka 28, amefunga magoli 64 katika michezo 104, na kulingana na umri wake inaonekana njia kuwa nyeupe kwake kuifikia rekodi ya Pele ikiwa atakazana ndani ya timu yake ya taifa.
Richarlson anayekipiga Everton ya England alifunga goli moja kwenye mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Estadio Nacional de Peru. Brazil na Argertina wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi 6 baada ya michezo miwili.
Msimamo wa wafunguji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Brazil uko hivi: Pele 77, Neymar 64, Romario 55, Zico 48, Bebeto 39, Rivaldo 35.
Ronaldo de lima Nazario.......
ReplyDeleteMtu m bad mbona simuoni kwenye hiyo list yako??