October 15, 2020


 SAHAU kuhusu umri wake wa miaka 33, imebainika kwamba thamani ya jembe jipya la Yanga, Saidi Ntibazonkiza raia wa Burundi ni kufuru kwani amewafunika nyota wote wa Bongo wakiwemo viungo wa Simba, Luis Miquissone na Clatous Chama.

 

Kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market, ambao unajihusisha na masuala mbalimbali ya wachezaji ikiwemo thamani zao, Ntibazonkiza ana thamani ya Euro 550,000 ambazo ni sawa na Sh bilioni 1.5, ikiwa hakuna nyota mwingine Bongo anayefikia kiasi hicho.


Nyota huyo wa zamani wa Vital’O ya Burundi, alitambulishwa Oktoba 12 na Yanga ikiwa ni usajili wao mpya baada ya kumpa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

 

Thamani ya Ntibazonkiza aliyefunga bao pekee la Burundi wakati ikicheza na Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki iliyopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Oktoba 11 inazidi ile ambayo ilitumiwa na Simba kusajili timu nzima msimu wa 2017/18, ambapo wenyewe waligota Sh bilioni 1.3.


 Ukiwajumisha nyota kama Aishi Manula, John Bocco, Erasto Nyoni na wengineo.

 

Wakati Ntibazonkiza akiwa na thamani hiyo Chama thamani yake ni Euro 100,000 (Sh 273,170,000) na Miquissone ni Euro 150,000 (Sh 409,755,000) kuonyesha kuwa jamaa huyo wa Burundi kawatupa mbali na kwenye timu za Bongo hakuna mchezaji ambaye mtandao huo unaonyesha kuwa anamfikia.

9 COMMENTS:

  1. Ila Yanga tuamimishwe tu kuwa kifungo chake cha kutokucheza mpira kwa miaka 5 kwa utovu wa nidhamu kimeisha

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Thamani hiyo ni ta mwaka gani?
    Msitufanye wajinga. Kuleta habari zisizo na mashiko ni kutufanya wajinga.
    Ni sawa na kuleta thamani ya Ronald De Lima ya mwaka 2002.
    Tuwekeeni thamani ya sasa.
    Kama mnadai thamani yake ni hiyo asingekuwa free player!
    Kukosa timu ni ushahidi kwamba hana thamani hiyo.
    Wacheni kulisha watu tango pori.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio waandishi wetu Hao kaka, wanachojua ni kupotosha tu ilimradi watu wengi wasome. Lakini hawaangalii athari za upotoshaji. Halafu Huyo waandishi atajisifu anajua miiko ya kazi yake.

      Delete
  4. Waandishi wengine bwana hewa sana

    ReplyDelete
  5. Kwani nyie yanga bado mnawaamini pengine huyo mchezaji hata mkataba hana ni filamu tu

    ReplyDelete
  6. duuuh yanga wamesajili mchezaji ghali mtandaoni hahahahahahah

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic