October 2, 2020


KLABU ya Yanga ipo kwnye mpango wa uongezea mkataba nyota wake wengine saba amba mikataba yao inakaribia kufika ukingoni.

Miongoni mwa nyota ambao wanakipiga ndani ya Yanga na mikataba yao inakaribia kuisha ni pamoja na:- Haruna Niyonzima, Mapinduzi Balama, Said Juma Makapu, Farouk Shikalo, Metacha Mnata, Abdulaziz Makame na Deus Kaseke.

GSM imepanga kuwaongezea fasta mastaa hao ili kuwazuia Simba wasiwachukue kama ilivyokuwa kwa Bernard Morrison raia wa Ghana ambaye aliichezea Yanga kwa miezi sita, kisha akajiunga na Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

 

Akizungumza jijini Dar, Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM na Makamu Mwenyekiti wa Usajili wa Yanga, Injinia Hersi Said, amesema kuwa zoezi hilo la kuwaongezea mikataba wachezaji wao wamepanga kulifanya kuwa endelevu.


Hersi amesema kuwa anaamini katika kikosi chao wapo baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao ipo mbioni kumalizika, hivyo kama wadhamini wamepanga kuhakikisha wanawabakisha kuendelea kukipiga Jangwani kwa lengo la kuiletea klabu mafanikio.


Aliongeza kuwa wachezaji hao watakaowabakisha ni wale wenye tija kwenye timu kwa kipindi chote walichoichezea Yanga bila ya kuangalia ukubwa wa jina lake.

 

“Huu mpango wa kuwaongezea mikataba tuliouanza tumepanga kuendelea nao siku za mbele ikiwa ni baada ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili beki wetu, Lamine Moro.

 

“Moro tumemuongezea mkataba baada ya kutambua mchango wake katika timu, hicho kigezo tulichokitumia kwake ndiyo tutakavyotumia kwa wachezaji wengine kuwaongezea mikataba.

 

“Tulianza kwa Moro, hivyo wachezaji wengine wanafuatia hivi sasa uongozi unapitia mkataba wa kila mchezaji kwa yule ambaye unakaribia kumalizika kwa kufuata vigezo vyetu, basi tutamuongezea mwingine,” alisema Hersi.

 

Ikumbukwe kuwa, GSM katika usajili wa dirisha kubwa msimu huu, ilihusika kwa kiasi kikubwa kushusha nyota wapya ndani ya Yanga.

 

Miongoni mwa nyota hao ni Carlos Carlinhos raia wa Angola, Michael Sarpong (Ghana), Yacouba Songne (Burkina Faso), Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ambao wote ni raia wa DR Congo.

4 COMMENTS:

  1. Hakuna mchezaji wa kuchukuliwa na simba hapo.

    ReplyDelete
  2. Sawa bt nini kinakukera au kutajwa Simba.

    ReplyDelete
  3. Kaseke huyo Nyota ya kukubalika mpaka aongezwe mkataba uko wapi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic