October 2, 2020

 


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa kwamba kimetokea malalamiko ya Klabu ya Yanga kuhusu uhalali wa mkataba kati ya mchezaji Bernard Morrison na Simba.


Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo imeeleza kuwa malalamiko hayo yanafanyiwa kazi.

Jana, Oktoba Mosi, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela aliweka wazi madai kuwa wamebaini mapungufu makubwa kwenye mkataba wa Morrison jambo ambalo wanahitaji haki itendeke.

Mwakalebelea alibainisha kuwa miongoni mwa mapungufu yalikuwa kwenye mkataba huo ni kutokuwepo kwa saini ya upande wa Simba pamoja na mashahidi jambo linalofanya mkataba huo uwe batili.

Morrison alikuwa mchezaji wa Yanga kwa msimu wa 2019/20 ambapo aliondoka ndani ya klabu hiyo kwa mvutano mkubwa kutokana na Yanga kudai kwamba ana mkataba wa miaka miwili huku yeye akieleza kuwa ana mkataba wa miezi sita.


9 COMMENTS:

  1. Hiyo kama kweli basi TFF ifuate sheria na i wa adhibu simba na kama uongo basi huyu mwakalebela akamatwe na ashtakiwe na pande zote za Simba na TFF. Ndipo watu kama hao watashika adabu za kuchafua mpira yaani na TFF leo ndio wataangalia mkataba ? Walikuwa wapi siku zote

    ReplyDelete
  2. Utopolo mzimu wa manji unawasumbua

    ReplyDelete
  3. Swali ninalojiuliza ivi inawezekana mkataba wa mchezaji usikaguliwe na TFF kipindi cha usajili? Mbona naona ngumu,kweli mkataba uwe na saini ya mchezaji pekee

    ReplyDelete
  4. Inawexekana and am really the man behind this movie is Mr senzo masingisa. Let's wait

    ReplyDelete
  5. TFF walimsajili kwa mkataba upi na ikizingatiwa mchezaji mwenyewe alikuwa kwenye mzozo mkali?

    ReplyDelete
  6. Senzo anadhani ni yeye tuu alikuwa na mamlaka ya kusaini mikataba. Hajui mpira wa bongo huyu. Hapa kwetu hata mimi nikiwa na pesa nasajili mchezaji yanga au simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Senzo kawaingiza chaka wakimalizana na Morison wanamgeukia yeye

      Delete
  7. Ivi kwa akili ya haraka unafkiri mchezaji aliewakana yanga kwa mkataba na kushinda kesi Simba itaachaje kumsainisha vipengele vyote wakati wanajua kabisa atawageuka mda wowote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic