October 2, 2020

 


ZIKIWA zimebaki siku 15 kabla ya Yanga kukutana na Simba, Uwanja wa Mkapa, Oktoba 18, viungo wawili wakigeni ndani ya Ligi Kuu Bara, Carlos Carlinhos wa Yanga na Luis Miqussone wa Simba wameingia kwenye vita ya kutengeneza mabao ndani ya timu zao.

Wakiwa wamecheza mechi tatu za ligi ambazo ni sawa na dakika 270, nyota hao wameonekana kushindana kutengeneza pasi za mwisho pamoja na kuwa wapigaji wa mipira iliyokufa ndani ya timu.

Carlinhos ametumia jumla ya dakika 137 na ametoa jumla ya pasi mbili ambapo zote ilikuwa ni kwa mipira ya kona iliyofungwa na Lamine Moro ambaye ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao mawili. Ilikuwa mbele ya Mbeya City Uwanja wa Mkapa na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri.





Kwa upande wa Luis ndani ya dakika 270 kwenye mechi zote tatu yeye ametengeneza jumla ya pasi nne ndani ya ligi ambapo ni moja alitoa kwa mpira wa kona wakati Simba ikishinda mabao 3-0 mbele ya Gwambina FC na nyingine tatu alitoa kwa Kagere na Clatous Chama wakati Simba ikishinda mabao 4-0 mbele ya Biashara United zote ilikuwa Uwanja wa Mkapa.

Vita yao itazidi kupamba moto hasa pale watakapokutana ndani ya uwanja Oktoba 18, mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau.


5 COMMENTS:

  1. ni upumbavu kumfananisha Miqussune na carlnho muwe mnaelewa mpira

    ReplyDelete
  2. Yan wandishi wetu wa habar n hovyoo kabsa,,wakikosa habar wanaamua kuandika ujinga tu ili watu wasome kumbe unajiharibia sifa zako za uwandishi,,Kama huna habari nzury sio lazma uwandike habar za kijinga

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli uandishi huu unakosa tathmini. Kweli aliye pata asilimia 80 na wa asilimia ishirini unaweza kuwashindanisha level moja? Hebu acha uandisha wa kisiasa kama vile unaogopa kutumbuluwa.

    ReplyDelete
  4. Waandishi wanatoa jasho lisilo la kawaida la kumpromote Carlinhos.Sioni jipya la huyu muangola.Kwa nini msitoe jasho la kumpromote Fei Toto?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic