MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameibuka na kusema kuwa kitendo cha uongozi wa Yanga kumsajili mshambuliaji, Saidi Ntibazonkiza wamefanya jambo sahihi.
Yanga Oktoba 12 ilitangaza kumsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akiwa huru baada ya Oktoba 11,2020 kufunga bao pekee katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars akiwa na timu ya Taifa ya Burundi katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.
Tambwe amesema kuwa, wapinzani wa Yanga watakuwa na kazi kubwa ya kupambana naye kwa kuwa anamjua vizuri ubora wake huku akisisitiza Yanga ilikosa mshambuliaji anayeweza kucheza namba kumi.
“Nimeona kwenye mitandao wanaandika lakini najua atawasaidia ila sijajua ni kocha mwenyewe ndiyo amependekeza au hiyo ni siri yao. Kuhusu mchezaji ni mzuri, anaweza kucheza kama winga wakati mwingine mshambuliaji wa kati.
“Najua atawasaidia kwa sababu ukiangalia wasifu wake amecheza katika ligi kubwa hivyo ana uzoefu wa kutosha, ukiona mtu anafika huko ujue anajua na kujua anajua kweli kwa sababu tulikuwa tunafanya naye mazoezi hapa Vital’O na siku nyingi tunajuana, nafikiri wapinzani wa Yanga haswa Simba watapata shida sana,” amesema Tambwe.
Kachaguliwa tim ya taifa kwa kuonekana mazoezini tu mchezaji mzuri lkn hakuwa na tim msim mzima watanzania tujifunze kitu
ReplyDeleteAlikuwa amefungiwa kucheza mpira kokote kwa miaka 5 sababu ya nidhamu mbovu
DeleteNakutupia goli la kufundishwa siyo la kufumba macho
ReplyDeleteTambwe ana uyanga na urundi huyu
ReplyDeleteInaonesha Tambwe ana usongo Sana na Mnyama. Maana anamsifia mno huyu BABU Said, ila muda utazungumza
DeleteKwa hiyo anadajiliwa kuisaidia yanga au kucheza na simba tuu?
ReplyDeleteAnasajiliwa
ReplyDeleteUtopolo mtaweweseka sana kwa Simba.
ReplyDeleteEmmy mtovu wa nidham, mchezaji naye mtovu wa nidham, ha!ha!haaaa, mwishowe mwalimu + mchezaji = utopolo wote watovu wa nidham
ReplyDeleteeti haswa simba hahahahaaa
ReplyDeletemwambieni huyo tambwe wakati vital'o wanapigwa 6 na yy huyo said alikuepo
ReplyDelete