October 15, 2020


 BONDIA bingwa wa mabara wa uzito wa superwelter, Hassan Mwakinyo atautetea mkanda wake wa Chama cha WBF Novemba 13 dhidi ya bondia wa Argentina Jose Carlos Paz.

Pambano hilo limepewa jina  la  'Dar Fight Night' limeandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.

Mbali ya kutetea mkanda huo, Mwakinyo pia atawania ubingwa wa mabara  wa uzito huo huo wa Chama cha IBA. Pambano hilo limepangwa kufanyika kwenye ukumbj wa Next Door Arena.

Mkurugenzi wa The  Jackson Group Sports, Kelvin Twissa amesema siku hiyo mabondia kutoka nchi tano watazichapa kumsindikiza Mwakinyo na Paz, akiwamo aliyekuwa bingwa wa dunia wa WBC, Fatuma Zarika kutoka Kenya.


Twisa amesema kuwa  Zarika atazichapa na Patience Mastara wa  Zimbabwe, na Zulfa Yusuph Macho atacheza na Alice Mbewe wa Zimbabwe.

Pia siku hiyo, bondia Abdallah Pazi maarufu kwa jina la Dullah Mbabe atacheza na Alex Kabangu wa DR Congo.


Alisema kuwa wameamua kuingia kwenye mchezo wa ngumi kutokana na kutambua vipaji vya mabondia mbalimbali hasa Mwakinyo ambaye anafanya vizuri katika mapambano yake.


"Siku hiyo kutakuwa na mapambano  makubwa ambapo mabondia kutoka nchi sita, Argentina, DR Congo, Kenya, Uganda, Zimbabwe na wenyeji Tanzania watapigana, ni siku ambayo mashabiki wa ngumi za kulipwa wataona kitu tofauti kabisa katika mchezo huo, " amesema Twisa.

 

Amesema kuwa kampuni yao chini ya udhamini wa Azam TV na Asas  ina uzoefu mkubwa katika kuandaa matamasha, masoko na shughuli mbalimbali na kuahidi kufanya jambo la kihistoria hapa nchini.

"Tunataka kuona mabondia wanaendelea kwa kupata mapambano mengi ya ngumi na kinacho endana na kazi yao, tulifanya kazi na Mwakinyo kwa miaka mitatu na kuona ufanisi wake, tumeamua kuendelea naye na mabondia wengine wa Tanzania, tutaubadili mchezo wa ngumi nchini," amesema.

 

Kwa upande wake, Mwakinyo amesema kuwa hiyo ni fursa kwake na kuahidi kufanya vyema siku hiyo.

"Namshukuru Twisa na kampuni ya Jackson Group Sports ambao wameonyesha nia ya kuubadili mchezo wa ngumi za kulipwa, sitawaangusha watanzania," amesema Mwakinyo.

 Mwakilishi wa WBF nchini Tanzania,  Chatta Michael amesema kuwa Rais wa shirikisho hilo, Goldberg Howard atasimamia mapambano hayo.

 

1 COMMENTS:

  1. Tunaomba mfuate taratibu za ngumi duniani,acheni siasa kwenye ngumi mnaboa kweli hasa kabla ya kuanza pambano,tofauti na mgeni rasmi utasikia tunamkaribisha mbunge,mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa pia tunatambua uwepo wa bwana tumbotumbo full siasa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic