October 3, 2020


 KIKOSI cha Simba leo kimewasili salama mkoani Dodoma baada ya kuanza safari leo mapema kwa basi kikitokea Morogoro ambapo kiliweka kambi jana, Oktoba 2.


Simba ina kazi ya kumenyana na JKT Tanzania kesho, Oktoba 4 mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni raundi ya tano.


Inakutana na JKT Tanzania ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Coastal Union mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao wanaamini kwamba utakuwa na ushindani mkubwa.


Simba yenyewe imetoka kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Gwambina FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa. 


Kwenye mchezo wa kesho atakosekana Gerson Fraga ambaye anasumbuliwa na majeraha aliyopata kwenye mchezo wake dhidi ya Biashara United uliochezwa Uwanja wa Mkapa.


Mchezo huo alitumia Fraga alimpisha nyota mzawa Said Ndemla ambaye kwa sasa ameitwa pia kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

7 COMMENTS:

  1. Kila heri Simba and a soon recovery wush to Fraga

    ReplyDelete
  2. Mikia wana vituko, eti Dodoma ni ugenini!!! Wakienda Mbeya wanasema wapo ugenini, wakienda Morogoro napo wanasema ni ugenini. Mwaka huu tutaona mengi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uneducated, manyani hawawezi kuelewa

      Delete
    2. Kwani Simba wanatumia uwanja upi kama uwanja wa nyumbani? Wewe unaonyesha unaipenda timu yako bila kujua utaratibu wa mpira ukoje...rudi shuleni ukasome...

      Delete
    3. Hata mechi ya Yanga vs Simba ya tarehe 18 , Simba wapo ugenini NYANI wewe

      Delete
  3. Wasio na vituko vya kila aina ni nani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kandambili aka gongowazi au vyura ambao Ni yebo yebo asilia

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic