UONGOZI wa Simba umesema kuwa ishu ya mkataba wa kiungo wao mshambuliaji, Bernard Morrison kwa sasa wanalifunga kwa kuwa hawana mamlaka ya kulizizungumzia.
Oktoba Mosi, uongozi wa Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela ulisema kuwa mkataba wa mchezaji huyo una mapungufu jambo ambalo wamelipekea Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF).
Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema:- "Sisi mechi yetu ambayo tunaitazama kwa sasa ni dhidi ya JKT Tanzania, unajua unawazuga 'fans' kwamba Mo kafanyaje 'haikrik', unazuga kwamba Kagere wamezinguana na kocha haiklik.
"Sijui unajaribu kuzuga kuwa mkataba wa Morrison sijui umefanyaje, haklik,hatuwezi kuondolewa mchezoni, sisi tupo vizuri. Unaendelea kuwazuga mashabiki kuwa ishu ya Morrison mmekata rufaa haiklik, ni rahisi kuwaongopea mashabiki kwa muda ila wakigudua watapata tabu.
"Nawausia tu kwamba waache kuwaongopea mashabiki watakimbiana watu, waongopee kwa muda, tuwaambie ukweli, watupe majawabu ya kinachowakera.
"Mjadala wa hili jambo la Morrison kwetu sisi tumelifunga huku tukiwaachia TFF na wenye mamlaka ambao wana kazi ya kutafuta majibu ya kile kinachozungumzwa.
"Kuhusu mkataba ni watu wawili hivyo tunaamini kwamba ikitokea ukweli ukapatikana ndio mamlaka zitajua namna ya kufanya.
"Simba tutamlinda mchezaji wetu kwa namna yoyote na mkataba ni siri kati ya mchezaji na mwajiriwa labda TFF wanaweza wakajua sasa sijui tunaelekea wapi kwenye maisha ya mpira, ila watengeneze majawabu ya kile wanachohitaji mashabiki.
Chanzo:Azam TV.
Tusubiri
ReplyDeleteNi kweli subira hapa ni muhimu. Kwa haraka haraka Yanga wanailaumu TFF kwa kuidhinisha mchezaji asiye na mkataba halali, inailaumu wizara kutoa kibali cha kazi kwa Morrison. Kifupi kwao wao mchezaji si halali japo aliidhinishwa na vyombo vinavyostahili kufanya hivyo. Je mkataba walioonesha ndio huo kweli mkataba halisi kati ya Morrison na Simba? Tuendelee kumywa supu, nyama ziko chini.
Delete