October 3, 2020

 




ZIKIWA zimebaki siku 14 kabla ya watani wa jadi Yanga na Simba kuonekana Uwanja wa Mkapa, rekodi zinaonyesha kuwa wachezaji wa kigeni wameuteka uwanja huo mazima ndani ya dakika 180 ambazo kila timu imetumia kwenye mechi zake.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic imevuna pointi nne kati ya sita kwa Mkapa huku ikifunga mabao mawili na kufungwa bao moja na Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck, imevuna pointi sita na kufunga mabao saba ambapo waliohusika kwenye ushindi wa timu zote mbili ni wachezaji wa kigeni.


Rekodi zinaonyesha kuwa wakati Yanga ikishinda bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa, Septemba 6, aliyetupia bao alikuwa ni Michael Sarpong raia wa Ghana alifunga baada ya mabeki wa Prisons kujichanganya.

Pia wakati Yanga  ikishinda bao 1-0 mbele ya  Mbeya City, Uwanja wa Mkapa, Septemba 13 aliyetupia bao alikuwa ni Lamine Moro raia wa Ghana kwa pasi ya Carlos Carinhos raia wa Angola.

Kwa upande wa Simba, mechi yao ya kwanza Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Septemba 20 dhidi ya Biashara United ilishinda mabao 4-0. Mabao ya Simba yalifungwa na Clatous Chama aliyefunga mawili kwa pasi ya Luis Miquissone , Meddie Kagere raia wa Rwanda kwa pasi ya Chama ambaye ni raia wa Zambia na Chris Mugalu raia wa Congo kwa pasi ya Luis raia wa Msumbiji.

Kisha ilicheza tena Septemba 26 dhidi ya Gwambina FC ilishinda mabao 3-0 watupiaji walikuwa ni Kagere kwa pasi ya Luis, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast kwa mpira wa adhabu ya faulo aliyechezewa faulo ni Rarry Bwalya raia wa Zambia na Mugalu kwa pasi ya Bernard Morrison wa Ghana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic