October 2, 2020

 


JUMA Mwambusi, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa ushindi wanaoupata kwenye mechi za ligi wa bao mojamoja utafika kikomo hivi karibuni kwa kuwa bado timu haijawa na muunganiko mzuri.

Yanga imecheza jumla ya mechi nne ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara na imefunga mabao manne ambao kwenye kila mechi imetupia bao mojamoja, kibindoni ikiwa na pointi 10 ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwabusi amesema kuwa ili wachezaji waweze kufunga mabao mengi ni lazima wawe na muunganiko mzuri jambo ambalo linafanyiwa kazi na benchi la ufundi.

“Kushinda ni jambo ambalo tunalihitaji na ili ufunge mabao mengi ni lazima timu iwe na muunganiko mzuri, kwa msimu huu ipo wazi wachezaji wengi ni wapya na muda wa maandalizi kabla ya msimu kuanza ulikuwa mfupi.

“Tunachokifanya kwa sasa ni kuendelea kutengeneza timu huku tukitafuta ushindi, bila kujali kwamba tunashinda mabao mangapi kwanza tunaanza kutafuta pointi tatu, kisha baada ya hapo tutakuwa imara kwenye kufunga mabao mengi kwa kuwa tutakuwa tumepata ule muunganiko mzuri.

“Wachezaji wanajua majukumu yao na kwa sasa kila mmoja yupo tayari kushindana, tutaimarika kupitia mazoezi tunayofanya pamoja na mechi nyingi za kirafiki,” amesema.

 Mchezo unaofuata wa ligi kwa Yanga ni dhidi ya Coastal Union ya Juma Mgunda utakaopigwa Oktoba 3, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.


Matokeo ya Yanga yalikuwa namna hii:- Yanga 1-1 Tanzania Prisons, bao la Yanga la Yanga lilifungwa na Michael Sarpong, Yanga 1-0 Mbeya City Uwaja wa Mkapa bao la Yanga lilifungwa na Lamine Moro, Kagera Sugar 0-1 Yanga, Mtibwa Sugar 0-1 Yanga bao lilifungwa na Lamine.

2 COMMENTS:

  1. Huo muunganiko mzuri mtaupata wapi Mzee Baba? maana ni mwezi sasa bado hamjaupata, kama haupo Tanzania uagizeni hata nje ya nchi. Tatizo umepata nafasi ya kujitetea chini ya kofia hiyo ya muunganiko mzuri, mnatumia kama kigezo cha kuwadanganya wana yanga waendelee kuwavumilia. Ukweli utadhiirika tu kwani mchezo wa soka uchezwa hadharani hauchezwi chumbani. Mimi kwa maoni yangu mmefeli hamna jipya na kibaya zaidi mnapata ushindi wa bahati bahati jambo linalo wafanya viongozi na mashabiki waendelee kuwaamini kwani kikubwa ni matokeo, lakini kwa mfumo na mpira unaochezwa Yanga, ipo siku mtaumbuka na kudhalilika sana, mtatamani mlikimbie benchi ili kuficha sura zenu. Hao wanao watetea watabaki kulialia kama makinda ya ndege yaliyofiwa na mama yao.

    ReplyDelete
  2. Tatizo la Yanga ni kutomtumia "kiungo mchezeshaji"; atakayepokea mipira kutoka kwa wakabaji na kuwachezesha washambuluaji. Katika mechi zote wametumika Fey, Zawadi na Mukoko ambao wote ni viungo wakabaji (wa kuzuia mashambulizi) hii inapelekea kutumia mashuti ya juu ya mbali kuvuka dimba la kati! Mipira ya aina hii inawapa kazi kubwa washambuliaji na kwa kiasi kikubwa kuwachosha.
    Mwambusi kama mzawa amsaidie Kocha Zlatko.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic