BAADA ya mechi nne kikosi cha muungano wa Yanga dhidi ya Simba ambao wanakutana Oktoba 18 Uwanja wa Mkapa kipo namna hii:-
Aishi Manula atakaa langoni kwa kuwa amecheza mechi zote nne ambazo ni dk 360 na ameruhusu mabao mawili ya kufungwa. Anakipiga Simba.
Shomari Kapombe uzoefu unambeba na amecheza mechi zote nne. Anakipiga Simba.
Mustapha Yassin pembeni atafiti kwani ameonekana kuaminika na benchi la ufundi anatoka Yanga.
Lamine Moro ataweza kuzuia na kufunga mechi tatu alizotumia dk 270 Yanga haijafungwa na amefunga mabao mawili.
Joash Onyango ni ingizo jipya limeweza kuaminika na Sven Vandenbroeck na kupewa majukumu kikosi cha kwanza yeye ni mzuri kwa mipira ya juu.
Luis Miqussone wa Simba ni kinara wa pasi za mwisho anazo nne kibindoni hivyo atakuwa mtengeneza mipango ndani ya kikosi.
Clatous Chama wa Simba mwendo wake ni mdogomdogo, ametupia mabao mawili na ana pasi mbili za mabao hivyo kazi yake itakuwa ni kufunga ama kutoa pasi.
Tonombe Mukoko wa Yanga ni mzuri kutengeneza mipango na kufunga anaweza, ana bao moja kibindoni.
Carlos Carinhos wa Yanga kazi yake itakuwa kupiga mipira iliyokufa ana pasi mbili za mabao na ni kinara kwa Yanga kwa kutengeneza pasi za mwisho.
Cris Mugalu ushkaji wake na nyavu licha ya kupewa muda mchache ndani ya ligi ametupia mabao mawili anatoka Simba.
Michael Sarpong mshambuliaji namba moja wa Yanga ni mpambanaji na hakati tamaa ndani ya uwanja ana bao moja kwenye ligi.
Upuuzi mtupu
ReplyDeleteTENA UPUUZI HASWA USHUZI MTUPU
ReplyDeleteHuyu mwandishi msenge kwel kwel
ReplyDeletekwa kweli ni upuuzi uliopindukia!
ReplyDelete