CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga leo anakazi ya kwanza kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo wa Lig Kuu Baa dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.
Hii inakuwa ni dabi yake ya kwanza baada ya kuibuka ndani ya ardhi ya Bongo akichukua mikoba ya Zlatko Krmpotic aliyefutwa kazi Oktoba 3.
Tayari amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi nne ambapo ameshinda tatu na kuambulia sare moja ambapo leo anatarajiwa kuwakosa nyota wake nane kwenye mchezo wa leo.
Ikiwa nafasi ya pili na pointi 23 baada ya kucheza mechi tisa inakutana na Simba iliyo nafasi ya tatu na pointi 19 nayo imecheza mechi tisa pia.
Kwa mujibu wa Kaze amesema kuwa atakosa huduma ya kiungo Carlos Carlinhos raia wa Angola ambaye anasumbuliwa na majeraha ya enka aliyoyapata kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania.
Kiungo huyo raia wa Angola amepiga jumla ya pasi mbili ndani ya ligi na kufunga bao moja akihusika kwenye jumla ya mabao matatu ya Yanga kati ya 11.
Mwingine ni Mapinduzi Balama ambaye yeye naye yupo nje tangu msimu uliopita akitibu majeraha yake ambayo aliyapata kwenye mazoezi wakati wa maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Ndanda.
Haruna Niyonzima naye pia yupo nje ya mpango wa Kaze kwa kuwa hakufanya mazoezi na timu kwa muda mrefu.
Wengine ambao inatajwa hawatakuwa sehemu ya kikosi kutokana na kutokuwa kwenye mpango wa Kaze ni pamoja na beki Paul Godfrey, kipa namba tatu Ramadhan Kabwili, Said Makapu na Abdulaziz Makame.
Pia mshambuliaji Juma Mahadhi naye anatajwa kukaa jukwaani akiwashuhudia wenzake wakipambania kombe Uwanja wa Mkapa.
Si Yanga tu na Simba pia kukosekana mshambuliaji uti wa mgongo bora Tanzania Kagere na nyota muhimu Fraga tegemo
ReplyDeleteNa pia Chama, Ajibu, Alefanya, Morison na wengineo
ReplyDelete