November 7, 2020


 LEO Kikosi cha Simba kitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu muhimu mbele ya watani zao wa jadi Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara huku kikikosa huduma ya nyota wake 7 wa kikosi cha kwanza.


Unakuwa ni mchezo wa kwanza kukutana kwenye dabi kwa mzunguko wa kwanza ambapo Yanga ni wenyeji na wapo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi tisa.


Watani Yanga wanaingia ndani ya uwanja wakiwa wanajiamini kwa kuwa mpaka sasa hawajapoteza mchezo ndani ya ligi wakiwa wameshinda mechi saba na kulazimisha sare mbili pointi zao ni 23.


Sven Vandenbroeck ambaye amelazimisha sare moja na kupoteza mechi mbili huku akishinda mechi sita na pointi zake 19 huenda akakosa huduma ya nyota wake hao wa kikosi cha kwanza kutokana na sababu mbalimbali.


Kwa mujibu wa Sven amesema kuwa nyota wake namba moja katika safu ya uchezeshaji, Clatous Chama ni miongoni mwa wachezaji ambao ni majeruhi.


Chama mwenye pasi tano za mabao akiwa amefunga mabao mawili pia kati ya mabao 21 ya Simba anatajwa kuumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Novemba 4 ambapo timu hiyo ilishinda kwa mabao 2-0.


Meddie Kagere pia yupo kwenye orodha ya wachezaji majeruhi akiwa ametupia mabao manne ndani ya ligi naye aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania wakati Simba ikishinda mabao 4-0.


Nyota mwingine ni Gerson Fraga huyu anasumbuliwa na goti na aliumia kwenye mchezo dhidi ya Biashara United atakaa nje msimu mzima.


Mshambuliaji namba nne ndani ya Simba, Charlse Ilanfya yeye hayupo kwenye mipango ya Sven hivyo atakuwa kwenye jukwaa akishuhudia wenzake wakipambana pamoja na kiungo Ibrahim Ajibu mwenye bao moja kibindoni ambaye hana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza leo.


Kiungo Bernard Morrison yeye hayupo kwenye mpango wa kikosi leo kwa kuwa amefungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) mechi tatu baada ya kumpiga Juma Nyosso kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shoting wakati Simba ikinyooshwa bao 1-0, Uwanja wa Uhuru.


Mechi yake ya kwanza kukaa jukwaani ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar na leo ni mechi yake ya pili.


Beki mzawa ambaye, Kened Juma naye pia atakosekana kwenye mchezo wa leo kwa kuwa ana mataizo ya kifamilia.


Kuhusu mchezo wa leo, Sven amesema kuwa wanaamini utakuwa ni mgumu ila watapambana kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

2 COMMENTS:

  1. Naomba niweke kumbukumbu vizuri Bernard Morison (mzee wa kuwachetua/kuwakela,{Bm3} ) huu utakuwa ni mchezo wake wa tatu kukaa jukwaani baada ya kufungiwa mechi tatu, mechi ya kwanza kukaa jukwaani ni dhidi ya Mwadui FC na mechi ya pili ni kati ya Simba Sc Vs Kagera Sugar na hii ni mechi yake ya tatu. Asante

    ReplyDelete
  2. Simba ni timu ya klabu bingwa Africa nikiwa kama shabiki wanachama wa simba ninawaomba wachezaji wetu wapigane kimataifa zaidi kwani hiyo ndio level yao. Wakikubali kulambishwa mchanga na utopolo wa matopeni hatuna budi dirisha dogo kufumua kikosi chote kwa ajili ya Africa champions league..Mkude,Ndemla,Dilunga hasa Dilunga ukicheza kama ulivyocheza na Nkana ya Zambia yanga watachomokaje? Mabeki wa yanga hawajapata fowadi wa kucheza nao maungoni kama washambuliaji wetu kesho wa simba watakuwa na ujasiri wa kuechezea mpira kwenye Box la Yanga basi kuna uwezekano wa yanga mucheza wachezaji pungufu kwa muda mrefu. Mpango ni kuwakera mabeki wao mapema tu ya mchezo wakose kujiamini waanze kucheza foul.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic