NYOTA wa zamani wa Klabu ya Simba, Mohamed Rashid ambaye kwa sasa maisha yake ya soka yapo ndani ya Klabu ya JKT Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed,’Bares’ amekuwa nje kwa muda mrefu akitibu majeraha ya nyama za paja.
Mshambuliaji huyo ameshindwa kucheza mchezo wowote kati ya 10 kwa msimu wa 2020/21 kutokana na kutibu majeraha hayo jambo ambalo limemkosesha furaha.
Akizungumza na Saleh Jembe, Rashid amesema kuwa hajawa na furaha kwa kuwa anapenda kucheza ila anashindwa kutokana na kuwa mgonjwa.
“Ukiwa nje kwa muda mrefu kwa mchezaji huo ni ugonjwa ila kwa sasa ninamshukuru Mungu nimeanza mazoezi jambo ambalo linanipa matumaini ya kuweza kurejea ndani ya uwanja,” alisema.
JKT Tanzania ipo nafasi ya 14, imefunga mabao 12 ilikubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Gwambina FC iliyo nafasi ya 10 na pointi 13 ikiwa imefunga mabao saba, zote zina pointi 10.
0 COMMENTS:
Post a Comment