PRINCE Dube mtupiaji namba moja ndani ya Bongo akiwa na mabao sita kwenye Ligi Kuu Bara na pasi nne za mabao mambo yamekuwa magumu kwa sasa ndani ya kikosi hicho baada ya kasi yake ya kucheka na nyavu kuzima ghafla.
Dube amehusika kwenye mabao 10 kati ya 15 ambayo yamefungwa na timu yake ya Azam FC, kibindoni ana tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba.
Miongoni mwa timu ambazo zimekutana na joto ya jiwe ya Dube ni Coastal Uniona aliwatungua mabao mawili, Kagera Sugar aliwatungua mabao mawili,Tanzania Prisons na Mwadui aliwatungua bao mojamoja.
Kwa sasa akiwa ndani ya Azam FC amecheza mechi tatu mfululizo ambazo ni dakika 270 na ameshindwa kutimiza jukumu lake la kufunga akiwa ndani ya uwanja.
Alianza kushuhudia timu yake ikisepa na pointi tatu mbele ya Ihefu kwa ushindi wa mabao 2-0 huku yeye akiwa mtengenza mipango kwa wachezaji wenzake yeye hakufunga.
Mchezo wa pili alishuhudia ngoma ikiwa nzito baada ya Azam FC kupoteza mchezo wake wa kwanza kuwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Moro.
Mambo yalizidi kukaza baada ya kukutana na JKT Tanzania Uwanja wa Azam Complex na kumfanya atumie dakika 270 bila kurejesha ushkaji wake na nyavu ndani ya Azam FC.
Vinara hao wa ligi wamecheza mechi 9 kibindoni wana pointi 22 mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Dodoma Jiji FC Novemba 5.
Na bado ndo maana watu walisema tumpe muda
ReplyDelete