KIKOSI cha Mwadui FC kimekuwa kwenye majanga baada ya kuyeusha pointi sita mfululizo kwa kupokea vipigo vikubwavikubwa.
Kikosi hicho kimeweka rekodi ya kukubali vipigo vikubwa mara mbili mfulizo ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.
Kwenye mechi hizo mbili mfululizo ambapo benchi alikaa Khalid Adam ameshuhudia vijana wake wakikubali kuokota nyavuni mabao 11 jambo ambalo linampasua kichwa kwa sasa.
Vijana wake walianza kuokota mabao 6 wakati wakikubali kichapo hicho mbele ya JKT Tanzania, Uwanja wa Mwadui Complex huku wao wakifunga bao moja pekee.
Balaa hilo liliwakuta tena jana, Oktoba 31 Uwanja wa Uhuru wakati wakiokota mabao 5-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa ligi.
Jumla Mwadui FC imefungwa mabao 19 ikiwa ni timu iliyobebeshwa zigo la mabao mengi kwa msimu wa 2020/21.
Ni Yanga pekee ambao wameweza kuwa na safu iliyoweka rekodi ya kuruhusu mabao machache kwa msimu wa 2020/21 ambayo ni mabao mawili.
Pia kinara wa utupiaji kwa mabeki anatoka Yanga ambaye ni Lamine Moro akiwa amefunga mabao mawili.
Adam amesema kuwa ni maumivu makubwa ambayo wanayapata kutokana na matokeo hayo jambo ambalo wanalifanyia kazi kwa mechi zao zijazo.
Itashuka tena uwanjani Novemba 4 Uwanja wa Mwadui Complex kumenyana na Ruvu Shooting.
0 COMMENTS:
Post a Comment