November 20, 2020

 


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa sasa una wasiwasi kuhusu kesi ya mchezaji wao Bernard Morrison huenda ikabadilishwa kwa kuwa dirisha dogo la usajili linakuja na hakuna walichopokea kuhusu malalamiko yao.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba Yanga waliripoti kwamba Morrison mkataba wake haujakamilika kwa kuwa kuna sehemu hazijajazwa na wahusika jambo linalomaanisha kwamba mkataba wake ni feki.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wanamashaka na kesi yao hiyo ambayo haijaskilizwa huenda mabadiliko yakafanyika kwenye mkataba dirisha dogo la usajili likifika.


"Kesi yetu kuhusu Morrison tulipeleka malalamiko kwa wahusika na mpaka sasa hakuna tulichokipata, wasiwasi wetu ni kwamba ikifika Desemba 15 dirisha dogo la usajili likifunguliwa huenda wakafanya mabadiliko.


"Kwenye mkataba wa mchezaji Morrison sisi tuliweka wazi kwamba kuna sehemu hazijazijajazwa hivyo huenda wakatumia mwanya huo kwenye dirisha dogo kuziba mapengo, maombi yetu ni kwamba shauri let lisikilizwe na lifanyiwe kazi," amesema Mwakalebela wakati akizungumza na Waandishi wa Habari muda huu makao makuu ya Yanga.

9 COMMENTS:

  1. Mmmmmmh mbona nahisi kama hekaya za abunuwasi hivi

    ReplyDelete
  2. Akumbushie na kesi yake ya kusema wanamsajili Chama wakati alikuwa na mkataba Simba

    ReplyDelete
  3. Nyie utopolo vipi mkataba wa morisson na simba unawahusi nn?kati ya morrison na simba kuna aliyelalamika?sakata la yanga na morrison alilalamika morison.Nyie nani mnalalamika?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani wewe ni TFF?Subiri TFF ndio alijibu hivyo unavyotaka wewe

      Delete
  4. Viongozi wa yanga wanastahili kuwa mirembe hospital

    ReplyDelete
  5. Na ile ambayo mlitaka kumsajiri chama wakati ana mkataba na simba nayo kumbusheni GONGOWAZI nyinyi

    ReplyDelete
  6. Utopolo narudia Tena na tena mzimu wa manji unawatesa

    ReplyDelete
  7. Baada ya kumkosa Chama mmerudi tena kwa Morrisson. Subirini na Mukoko achukuliwe ndio akili itawakaa sawa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic