November 20, 2020

 


NOVEMBA 21, Simba chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union ya Juma Mgunda, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. 


Simba ikiwa nafasi ya tatu inakutana na Coastal Union iliyo nafasi ya 10 ambapo Coastal Union imekusanya pointi 12 na Simba imekusanya pointi 20.


Tatizo la Coastal Union ni safu ya ushambuliaji ambayo imefunga jumla ya mabao 7 inakutana na ile ya Simba ambayo imefunga mabao 22.


Kwa upande wa safu ya ulinzi ile ya Coastal Union iliyo na Hance Masoud imeruhusu mabao 10 na Simba ambayo pembeni yupo Mohamed Hussein imeruhusu mabao matano.


Coastal Union chini ya Juma Mgunda itatumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa sababu Uwanja wa Mkwakwani umefungiwa ili ufanyiwe maboresho.


Vita yao ni kwenye kusaka pointi tatu muhimu kwa kuwa kila timu inazipigia hesabu pointi hizo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic