November 25, 2020


 KIKOSI cha Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kimewasili Abuja kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa unaotarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 27-29.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Jos unaotumia na timu hiyo ya Nigeria.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa kati ya Desemba 4-6.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa wanatambua wanakwenda kupambana na timu yenye wachezaji wazuri hasa kwenye nafasi ya ushambuliaji jambo litakalomfanya aongeze umakini.

"Wapinzani wetu ni wazuri hasa katika nafasi ya ushambuliaji, imani yetu ni kwamba tutafanya vizuri hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti," amesema.

5 COMMENTS:

  1. Yani mpk leo hamjui mechi inachezwa lini

    ReplyDelete
  2. Mechi zote tulizocheza kipindi hicho Na Enyimba katika mji WA ABA tulicheza ijumaa.Sijajua kwnn ukasema jpili.Wengi kule Waislam.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mechi jpil saa 12:00 jioni Tz time kule saa 10:00 jion

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic