JUMA Mwambusi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa tatizo kubwa la washambuliaji wa kikosi hicho ni kukosa utulivu wakiwa ndani ya 18.
Yanga ambayo imecheza jumla ya mechi 11 kwenye ligi imefunga mabao 13 na kinara wa utupiaji ni Michael Sarpong mwenye mabao matatu kibindoni.
Leo Novemba 25 ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC ambayo safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 18 na kinara wao ni Prince Dube mwenye mabao sita.
Timu zote zina pointi 25 kibindoni hivyo ili Yanga ijihakikishie nafasi ya kukaa kileleni leo ni lazima ishinde ikiwa italazimisha sare basi itabaki nafasi ya pili.
Kinara wa utupiaji ndani ya Yanga ni Michael Sarpong mwenye mabao matatu akiwa amecheza mechi 10 kati ya 11.
Mwambusi amesema kuwa:”Kuna tatizo la utulivu kwa safu ya ushambuliaji ikiwa eneo la 18 hilo tumeliona na tunalifanyia kazi malengo yetu ni kuona kwamba washambuliaji wanatumia nafasi ambazo watazipata.
“Imani yetu ni kwamba kwa namna ambavyo tunawafundisha wanaelewa taratibu na kasi itakuwa kubwa kwenye mechi zetu zijazo,” .
Mimi nilifikiri kocha mkuu wa Yanga ni Kaze lakini ndio leo nimejuwa sio yeye Bali ni Mwanbusi
ReplyDeleteMwandishi mavi
ReplyDeleteMmesajili wachezaji gani sasa wa kimataifa ambao hata utulivu hawana.... Nadhani hata makocha hawajui yatizo ni nini maana tatizo hili ni la muda mrefu
ReplyDeleteHawajazoweana wakizoweana magoli ya kumwaga
ReplyDelete