November 19, 2020


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kusaka pointi tatu mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Novemba 22, Uwanja wa Mkapa.


Mchezo huo wa raundi ya 11 unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu hizi mbili kutokana na rekodi zao walipokutana kwa msimu wa 2019/20 zama zile za Hitimana Thiery.


Mechi zote mbili ambazo ni dakika 180, Thiery ambaye kwa sasa amefutwa kazi waligawana pointi mbili walipokuwa wakisaka pointi sita ambapo mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 na ule waliokutana Uwanja wa Majaliwa walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.


Wanakutana Uwanja wa Mkapa, Novemba 22 kila timu ikiwa na kocha mpya ambapo kwa Yanga wao wanaye Kaze ambaye alichukua mikoba ya Zlatko Krmpotic na Namungo wanaye Hemed Morocco ambaye amechukua mikoba ya Thiery.


Kaze amesema:"Tunahitaji kupata matokeo chanya kwenye mechi zetu zote na nina amini kwamba wachezaji wanalijua hilo na watapambana kupata matokeo," amesema.


Morocco amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa watapambana kupata matokeo.


Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa imekusanya pointi 24 kibindoni inakutana na Namungo ikiwa na pointi 14 nafasi ya tisa.


Ukuta wa Yanga umeruhusu mabao matatu na ule wa Yanga umeruhusu mabao matatu.

1 COMMENTS:

  1. Ukuta wa yanga umeruhusu mabao 3 na ule wa yanga mabao 3,hii inamaana gani?muwe mnahariri habari zenu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic