JAMHURI Kiwhelo, ‘Julio’ Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes amesema kuwa wapo tayari kupeperusha bendera ya Taifa kwenye mashindano ya Baraza la Michezo Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Mashindano hayo ambayo yatashirikisha timu nane ambazo ni Tanzania ambao ni wenyeji, Zanzibar, Somalia, Djibout, Kenya, Uganda, Burundi, Ethiopia na Sudan ya Kusini yatafanyika mkoani Arusha kuanzia Novemba 22.
Akizungumza na Saleh Jembe, Julio amesema kuwa wanaamini watafanya vizuri kutokana na maandalizi kuwa mazuri katika kila namna.
“Tupo vizuri tayari tumekwisha kutia kambi Karatu huku, wachezaji naona wanafurahi kila mmoja na hilo linatoa picha kwamba hakuna kitakachoharibika tutafanya vizuri hivyo mashabiki waendelee kutupatia sapoti.
Wakati wa maandalizi Ngorongoro ilicheza mchezo wa kirafiki na Sudan Uwanja wa Uhuru na ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Uhuru.
“Makosa ya timu kupitia mechi zilizopita tumeyaona na tutayafanyia kazi, kikubwa ni kuona kwamba kila mmoja anatimiza majukumu yake kwa wakati na kila kitu kitakuwa sawa,” amesema Julio.
0 COMMENTS:
Post a Comment