December 25, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hali ya nyota wao kipenzi cha mashabiki, Mapinduzi Balama kwa sasa inaendelea vizuri na muda wowote kuanzia sasa anaweza kurejea Bongo.


Nyota huyo ambaye anakumbukwa kutokana na kuanza kuweka mzani sawa kwenye Dar Dabi ya mabao 2-2 dhidi ya Simba kwa kumtungua Aishi Manula bao la nje ya 18.

 

Msimu wa 2020/21 amekuwa nje mpaka wakati huu wa raundi ya 17 kutokana na kutibu majeraha yake ili aweze kuwa fiti.


Mapinduzi alipelekwa Afrika Kusini hivi karibuni kupatiwa matibabu kutokana na kuvunjika mguu tangu msimu uliopita alipokuwa mazoezini.

 

 Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa, tayari kiungo huyo anaendelea vyema na matibabu na wiki ijayo akitarajiwa kurudi hapa nchini.

 

"Mapinduzi anaendelea vizuri, tumewasiliana na madakari wake wamesema anaendelea vyema na tayari ameshafanyiwa upasuaji, wiki ijayo anatarajia kurejea nchini,” amesema Mwakalebela.

6 COMMENTS:

  1. Sasa hivi Morison amehama mmegeuzia kibao mapinduzi ile kauli ya Eymael ilitakiwa kuwalenga na nyinyi waandishi wenye mahaba na utopolo

    ReplyDelete
  2. Kwahyo amekukera 😂😂😂 na watawakera sanaaa veteran fc

    ReplyDelete
  3. Mtu kavunjika mguu mmemuweka muda wote huo bila matibabu ya uhakika... Mungu amsaidie tu apone Ila Utopolo hawajielewi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nani kakwambia alikuwa hatibiwi? Mkia mbeleko.. kihoro kitawatesa

      Delete
    2. Utopolo wagumu sn kuelewa.... Soma vzr

      Delete
    3. Bora wao wanatibu wachezaji wao uliko nyie mikia, mchezaji akiumia mnamtelekeza. Fraga majeruhi mmeamuacha, sasahivi Kagere mnamtumia ila mnasema atatibiwa na chama cha soka cha Rwanda. What a shame

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic