December 14, 2020


 LIGI ya Kikapu nchini Marekani (NBA) imetangaza kusitisha mchakato wa kuwapima wachezaji matumizi ya bangi kabla ya msimu wa 2020-21 kuanza kama ambavyo taarifa ilivyotolewa awali.

 

NBA na NBPA kwa pamoja wameafikiana maamuzi hayo ya kutofanya vipimo vya matumizi ya bangi, baada ya taarifa kutoka umoja wa mataifa ambazo zinadai kuwa mmea wa bangi hauna madhara mwilini na unasaidia kuponya baadhi ya magonjwa.


Hivyo NBA wakaamua kusitisha zoezi hilo, lakini wakasisitiza kuwa vipimo vya kubaini matumizi mabaya ya dawa za kulevya na kuongeza nguvu michezoni vitaendelea kama kawaida na wachezaji wanapaswa kuchukua tahadhari.

 

Hii inakuja pia kufuatia baadhi ya majimbo nchini Marekani kuendelea kuruhusu matumizi ya bangi kwa matibabu ya mwili, hivyo NBA wameonelea pia kutoendeleza sheria ya kuwapima wachezaji wao kwa kuwa itakuwa haina maana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic