UKITAJA timu zenye kila kitu ndani ya ardhi ya Tanzania kwa
wakati huu ukiliweka kando jina la Klabu ya Azam FC ni kosa kubwa kabisa.
Nasema ni kosa kubwa kwa sababu utakuwa umeiweka kando
timu ambayo ilikuja kufanya mapinduzi kwenye masuala ya mfumo pamoja na mwendo
wa timu zetu Bongo.
Weka kando Gwambina FC ambayo nayo pia inazipeleka darasani timu
kongwe ikiwa ni Yanga na Simba katika masuala ya umiliki wa uwanja.Uwanja wa
Gwambina unaitwa Gwambina Complex.
Sema Azam FC ile ambayo ilianza kwa kasi msimu wa 2020/21.
Mechi 7 mfululizo bila kuonja tamu ya kupoteza pointi tatu, nini tena unataka.
Usajili ghali ambao ulifuata taratibu zote kuanzia vipimo mpaka
CV za wachezaji, hakika Azam FC hapo ilileta utamu ule ambao wengi walikuwa
wanausubiri ndani ya Ligi Kuu Bara.
Prince Dube usajili wake ulijibu,alitajwa kuwa mrithi wa kiatu
cha ufungaji bora anayekipiga ndani ya Simba Meddie Kagere hapo walifanya jambo
zuri ila alipopata majeraha ngoma imekuwa nzito.
Ghafla mambo yamebadilika kutoka kuwa timu isiyofungwa sasa
inakuwa timu inayopambana kupata sare ndani ya uwanja.
Tazama mechi tatu mfululizo ambazo Azam FC imepata pointi
mojamoja. Ilianza kwa Biashara United ikiwa ugenini ikaibukia kwa Gwambina FC
ngoma ni pointi mojamoja.
Wamerejea nyumbani, Uwanja wa Azam Complex wakiwa na imani ya kusepa na pointi tatu muhimu mbele ya Namungo FC, utamu ukakata mwishoni.
Sare ya mabao 2-2 dhidi ya Namungo FC sio jambo baya kwa sababu
ni matokeo ndani ya uwanja ila hapo tatizo linakuja nini wanakosa Azam FC.
Azam FC bila ya Dube haipati matokeo, Azam FC yenye kila kitu,
ile yenye uwanja bora ndani ya Bongo, yenye wachezaji inaowahitaji leo hii inapambania
sare ndani ya uwanja.
Bado kuna muda wa kujipanga ili kufanya vizuri ila ni somo kwa
timu nyingine kumtengeneza mchezaji mmoja kuwa mwenye jukumu la kuicheza timu
ni kama ilivyo kwa Simba asipokuwepo Clatous Chama basi matokeo inayaskia
kwenye bomba.
Bado kuna nafasi kwa Azam FC kufanya maboresho na kuzidi kuwa imara kwa kuleta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara.
Pia hata mwendo wa Ihefu FC pamoja na Mwadu bado inaonekana hawajashtuka kwa wakati huu ni muhimu kufanya maboresho ili kuwa imara ndani ya uwanja.
Ili uweze kufanikiwa katika mpira unahitaji vitu vitatu ambavyo ni Uongozi bora, rasilimali/uwekezaji pamoja wachezaji bora. Azam wanafail kwenye uongozi bora na wachezaji wa kiwango cha juu. Wao wanaamini kili kinachotamkwa Yanga au kupita Yanga ni bora jambo ambalo si kweli!! Wasipotoka kwenye vivuli vya Yanga na Simba wataendelea kuwa washiriki tu
ReplyDeleteNi sahihi. Wanaangukia kwenye ushabiki wa Simba na Yanga..Hawajiamini kama peke yao wanaweza bila kutegemea hizo timu kongwe
Delete