December 17, 2020

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Simba, Meddie Kagere amefanikiwa kuandika rekodi ya kufunga mabao 50 ndani ya Ligi Kuu Bara tangu alipojiunga rasmi na Simba, msimu wa 2018/19.

Mshambuliaji huyo amefanikiwa kuandika rekodi hiyo baada ya kufunga bao la mkwaju wa penalti dhidi ya KMC usiku wa kuamkia leo, mchezo ulioisha kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kagere alikamilisha rasmi usajili wake ndani ya Simba Juni 27, mwaka 2018 ambapo ndani ya misimu miwili iliyopita amefanikiwa kuibuka na tuzo ya mfungaji bora, 

Kagere alianza kampeni yake ndani ya Ligi Kuu Bara msimu  wa 2018/19 ambaqpo alimaliza akiwa ameweka kambani mabao 23, msimu uliofuata yaani 2019/20 Kagere alifanikiwa kuweka kambani mabao 22 huku msimu huu mpaka sasa akiwa tayari ameweka kambani mabao matano hivyo kufanya jumla ya mabao 50.

Kati ya mabao hayo 50 Kagere amefunga mabao 28 kwa guu lake la kulia, mabao nane kwa guu lake la kushoto huku mabao 14 akifunga kwa kutumia kichwa.


  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic