December 25, 2020

 


NYOTA wa Klabu ya Al Ittihad na timu ya Taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi ambaye ni mshambuliaji leo anatimiza miaka 28.

Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia,  Okwi ameletwa duniani Desemba 25,1992 huko nchini Uganda.

Kwenye maisha yake ya soka aliweza kupita ndani ya Klabu za Simba na Yanga kwa nyakati tofautitofauti.

Alisajiliwa na Simba msimu wa 2010-13 akitokea Klabu ya SC Villa ambapo alikuwa amecheza jumla ya mechi 40 na kutupia mabao 13.

Msimu wake wa kwanza ndani ya Simba alicheza jumla ya mechi 38 na kutupia mabao 18, alisepa Simba na kujiunga na Klabu ya Etoile du Sahel msimu wa 2013 hakudumu akajiunga na SC Villa kisha Yanga msimu wa 2013-14 ambapo alicheza jumla ya mechi 18 na kutupia mabao 9.


Alirejea tena ndani ya Simba msimu wa 2017-19 ambapo alicheza jumla ya mechi 53 na kutupia mabao 36 kwa sasa yupo ndani ya Al Ittihad ya Misri ambapo amecheza jumla ya mechi 14 na kutupia mabao mawili.



12 COMMENTS:

  1. Hivi wachezaji na wasanii wa ukanda wetu umri wao huwa unarudi nyuma badala ya kwenda mbele au?

    ReplyDelete
  2. Sawa na mimi maana mimi nimezaliwa tarehe 25 mwezi 12 mwaka 1992 by Rashidi maona (Messi)

    ReplyDelete
  3. Sasa Kama kwa hali hiyo miaka 28, je akifikisha miaka 38 si atakuwa baby kabisa??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukitaka kujua uongo wao waulize walianza darasa la kwanza mwaka gani halafu fanya hesabu ya mwaka aliozaliwa utakuta mtu alianza darasa la kwanza akiwa na mwaka mmoja au miaka miwili.Kuna mwaka nilisoma mahojiano ya golikipa mmoja mkongwe umri alioutaja ukitoa na mwaka alioanza darasa la kwanza nikakuta alianza darasa la kwanza akiwa na mwaka mmoja

      Delete
  4. HII INA MAANA MCHEZAJI KAMA C. Ronaldo ni mkubwa kuliko Okwi, Jakaya alisema:- "AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO"

    ReplyDelete
  5. Kwa hiyo okwi na Samatta wapo Sawa dadeki zao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu Okwio ni kibabu ila kadanganya umri, kama unafanya mazoez na una sura y kizee hivyo, je, angekuwa kitaa?

      Delete
    2. Na cha ajabu samamtta atastaafu mpira atamuacha okwi anacheza muhimu malengo mzee

      Delete
  6. OKWI aliwadanganya mikia fc ili wamsajili ila kiufupi ni mkubwa kuliko hata Samatta

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lakini hata Yanga walimsajili, au umesahau? Unataka kusema aliwadanganya Simba halafu akawaambia ukweli Yanga? Halafu akalamba mamiioni ya Yanga, akafanya vituko, hata miezi sita haijaisha akarudi Simba!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic